MAMBO 10 USIYOYAJUA KUHUSU DIAMOND PLATNUMZ

Show ya Mkasi ya wiki iliyopita imetufanya tufahamu mambo 10 muhimu tusiyoyajua kutoka kwa Diamond kama ifuatavyo:

1. Yupo kwenye mazungumzo na label moja kubwa duniani ambao walimtafuta baada ya kufanya show ya Big Brother Africa.

2.Ana simu nne na moja ina line mbili, hivyo ana line tano.Simu yake huiweka silent muda wote kwakuwa zinapigwa muda mwingi. Anayo moja maalum ambayo watu wengi hawaijui.

3. Ana nyimbo 133 ambazo ameshazirekodi tayari.

4.Mama yake alikuwa anampeleka kwenye talent show na kumsubiria hadi usiku mpaka aperform ndo wanarudi wote. Ndugu zake wengine waliona anamdekeza mwanae.

5.Zamani alikuwa anapenda kurap lakini aliona ukirap huwezi kupata mademu. Alipokuwa akiimba watu wengi walikuwa wanamkataza kwakuwa waliona hawezi.

6. Q Chilla ndiye msanii anayempenda zaidi na muda mwingi husikiliza nyimbo zake.

7. Anamaliza mjengo wake uliopo Tegeta Dar es Salaam.

8.Anapenda kuja kuwa kama Usher Raymond.

9.Anapenda jinsi Dully anawasupport wasanii wachanga kwa kuwashauri na kuwapa moyo kuliko wasanii wengine wakongwe ndo maana anasema huwa hachuji.

10.Maproducer anaowazimia Tanzania Manecky, KGT, Manwalter na Marco Chali.

6 comments:

Anonymous said...

diamond kazi yako nzuri na uko kikazi zaidi, punguza skendo za mademu zinakushusha uthamani

Anonymous said...

Hongera sana diamond unajitahidi ila kumbuka Mungu ndiye mweza wa yote mrudie mungu wako atakupa zaidi na zaidi wasichana hawakusaidii kitu zaidi ya kukumaliza kimwili na kiroho braza.

Anonymous said...

Kaza buti Mnyanyema safari bado ndefu ukizingatia upo kwenye usanii kwa malengo gani basi utafanikiwa kaka kazi zako zinakubali big up

countryboy veer said...

Upole
wangu simanzi Eeeh!
Kwangu
kupenda maradhi iiih!
Lakini
kupendwaga mi nae bahati
huwaga sina...
jichoni
kwangu kibanzi Eeeeh!
ninakapenda
kamanzi Iiih!
Oooh Licha
ya kumthamini kama
shilingi tatizo hata raha
sina....
Ufinyu wa
mboni zangu, unatazama
mengi yanayonipa mateso,
Ukweli
hatakupenda sina raha! ona
nakonda kwa mawazo.
Masikini
penzi langu jina lishakatwa
na kauli roho inatoka kesho
Kutwa nzima
mara Eeeh! Mara Iiiiii! Hata
najuta kupenda....

Anonymous said...

Msanii kazi umeiweza achana na mademu wanakuua kisanii hujengi kijana jipange na demu mmoja funga nae ndoa heshima na kazi utalinda sana hadhi yako. congrats

acemaxskulitmanggis.com said...

obat penyakit sinsitis
i like youe post and thank's for your information
very nice ^___^
obat darah tinggi
Pengobatan Batu Empedu